How to Identify Forest Crime: Africa - Swahili

1. Zingira sehemu ya nje ya eneo la uhalifu ili wewe na wenzako mlisiliathiri. Egesha magari umbali wa angalau mita 100. Usisogeze chochote. KUENDESHA MASHTAKA DHIDI YA MSHUKIWA BAADA YA KUMKAMATA 3. Tayarisha mchoro sahili wa eneo la uhalifu, ukionyesha mahali halisi au uhusiano kati ya vitu vilivyomo na ushahidi. 4. Rekodi nyayo zozote, viatu au ishara zozote zinazodhibitisha kilichofanyika AU zinazomhusianisha mshukiwa na eneo hilo la uhalifu. 5. Kamata au kusanya kitu chochote ambacho unadhani kinahusiana na eneo la uhalifu, ikiwezekana kwa kutumia penseli, glavu au kijiti. Weka vitu katika mifuko tofauti tofauti au kwenye karatasi iliyokunjwa. 6. Tayarisha ripoti fupi au andika maneno makuu ukiwa katika eneo la uhalifu na jumuisha kitu chochote kinachoweza kuhesabiwa, kwa mfano, alama za nyayo, vitu vilivyokamatwa (silaha, risasi, vifaa vya kukatia, vipande vya wanyama wa porini, mifuko ya mkaa au magogo), na watu walioko -- pamoja na tarehe, saa, na muda uliokadiriwa kupita tangu tendo la kihalifu lilipotokea, muda uliotumia katika eneo la uhalifu, maelezo kuhusu eneo hilo na/au alama ambatanifu za kijiografia (coordinates). Hakikisha kwamba habari zinazokusanywa zitatosha kulipata eneo hilo tena. 2. Piga picha.

19

Made with FlippingBook - professional solution for displaying marketing and sales documents online